.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 1 Januari 2017

HARRY KANE NA DELE ALLI WAITAKATISHA TOTTENHAM SPURS

Harry Kane na Dele Alli wamefunga magoli mawili kila mmoja wakati Tottenham ikiichakaza Watford kwa magoli 4-1 na kutinga katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.

Katika mchezo huo Tottenham Spurs iliutawala mchezo huo wakipiga mashuti 13 golini katika kipindi cha kwanza, huku Harry Kane akiwa wakwanza kufunga goli punde tu baada ya shuti la Alli kugonga mwamba.

Kane tena alifunga goli la pili ambalo linamfanya kufikia rekodi ya magoli 59 ndani ya michezo 100 ya Ligi Kuu ya Uingereza sawa na Therry Henry, kisha Alli akafunga goli la tatu na kumalizia goli la nne katika dakika ya 46.
                                   Harry Kane akiachia shuti kati kati ya mabeki na kufunga goli
             Dele Alli akifunga goli katika mchezo huo baada ya kumzidi maarifa kipa Gomes 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni