Kikosi cha vijana wa Liverpool
kimejikuta kikidhibitiwa na kutoa sare tasa na timu ya daraja la pili
ya Plymouth Argyle katika mchezo wa raundi ya tatu wa kombe la FA
katika dimba la Anfield hii leo.
Wenyeji Liverpool ambao wachezaji
wake walikuwa na wastani wa miaka 21, walimiliki mpira kwa asilimia
80.3 katika kipindi cha kwanza huku Sheyi Ojo akishindwa kutumia
nafasi nzuri kufunga.
Katika mchezo huo Divock Origi pia
goli lake lilikataliwa kutokana na kumchezea rafu Gary Miller, kabla
ya kocha Jurgen Klopp kuamua kuingiza kikosi cha kwanza cha kawaida
cha kina Daniel Sturridge, Adam Lallana na Roberto Firmino.
Mpira uliopigwa na Sheyi Ojo ukidakwa na kipa
Jitihada za Divock Origi zikigonga ukuta wa timu ya Plymouth
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni