Kapteni wa Chelsea, John Terry
ametolewa nje kwa kadi nyekundu wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi
wa magoli 4-1 dhidi ya timu ya ligi ya daraja la kwanza ya
Peterborough katika mchezo wa kombe la FA.
Katika mchezo huo Chelsea ilifanya
mabadiliko ya wachezaji tisa, na nusura wajikute wakiwa nyuma baada
ya Asmir Begovic kuokoa mpira wa kichwa cha karibu uliopigwa na Lee
Angol.
Hata hivyo kikosi hicho cha Antonio
Conte, kilipata goli la kwanza kupitia kwa Pedro, kisha Michy
Batshuayi kufunga la pili na Willian kufunga la tatu baada ya
mapumziko kabla ya Pedro.
Pedro akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la kwanza katika mchezo huo
Tom Nicholas akiangali mpira alioupiga ukielekea kutinga kwenye goli la Chelsea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni