Mchezaji kiungo John Mikel Obi
ameingia katika orodha ya nyota wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza
waliohamia Ligi Kuu ya China baada ya kuthibitishwa uhamisho wake kwa
klabu ya Tianjin TEDA.
Picha iliyotumwa kwenye tovuti ya
China ya Webo, inamuonyesha mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea Mikel
akipeana mkono na afisa wa klabu ya Tianjin huku akiwa na fulana ya
timu hiyo.
Mikel, aliyejikuta akiondoka Chelsea
msimu huu akikosa nafasi kutokana na kuwa na wachezaji kama N'Golo
Kante, Nemanja Matic, Nathaniel Chalobah na Cesc Fabregas, atalipwa
paundi 140,000.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni