Mshambuliaji wa Leicester City Riyad
Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika inayotolewa
na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Mchezaji huyo raia wa Algeria ambaye
aliisaidia Leicester kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza, pia ni
mchezaji bora wakulipwa wa Afrika na Mchezaji Bora wa Mwaka wa BBC
Katika tuzo hizo mchezaji wa
Borussia Dortmund, raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang alishika
nafasi ya pili na mshambuliaji wa Liverpool Msenegal Sadio Mane wa
tatu.
Mchezaji wa Arsenal raia wa Nigeria
mshambuliaji Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
kijana.
Mchezaji wa Arsenal Alex Iwobi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni