.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 9 Januari 2017

KOREA KUSINI YAITAKA BUSEGA IWEKEZE ZAIDI KWENYE AFYA YA MAMA NA MTOTO.

 
Balozi wa Korea Kusini, Song Gerum Young akiwa na Mbunge wa Busega, Mh Raphael Chegeni 
                                                                                      
                                                                                                Na Shushu Joel,BUSEGA.

RASLIMALI watu kwa maana ya ya idadi ya watu ni moja ya viashiria vya ustawi wa taifa lolote lile hapa duniani.

Taifa lolote lile lenye idadi kubwa ya watu kimsingi,linatarajiwa kuwa na ustawi mkubwa katika suala zima la maendeleo ili taifa hilo liweze kukua na kujilinda na afya iliyo bora kwa wale ambao linawategeneza ili waweze kukuza uchumi huo.

Na ndio maana ukitaka kufumbua zaidi,unaweza kungalia uhalisia ulivyo kwenye baadhi ya mataifa yaliyo na idadi kubwa ya watu duniani.

Mataifa hayo yanaongozwa na China yenye watu zaidi ya bilioni 1.3 huku nyuma ikifuatiwa na nchi ya India yenye watu wapatao billion 1.2 na kisha kufuatiwa na nchi ya Marekani yenye watu wapatao million 400.

Mataifa hayo yote kimsingi ndio yaliyo na uchumi mkubwa zaidi duniani, yakiongozwa na Marekani na kufuatiwa na China.

Hata India nayo iko kwenye kundi la mataifa yanayoibukia kwa kasi katika uchumi maarufu kama BRIC, yaani Brazil,Urusi,India na Uchina yenyewe.

Kwa hali hiyo taifa lenye idadi kubwa ya raslimali watu,lazima katika kipindi Fulani lipige hatua kubwa kimaendeleo na kama si leo basi siku za usoni.

Sababu kubwa ya mataifa haya kuweza kupiga hatua kimaendeleo ni kile kitendo cha mataifa hayo kuwekeza nguvu nyingi katika kundi la watoto wadogo na kina mama kwani wao ndio nguzo pekee inayoonekana kuongeza uchumi katika mataifa hayo.

Maneno hayo yalisemwa juzi na balozi wa Korea Kusin,i Song Gerum Young alipokuwa akisaini mkataba wa serikali ya Korea kuweza kusaidia wilaya ya Busega ili kuondokana na wimbi kubwa la kupotelewa kwa raslimali watu ambao upoteza maisha katika wilaya hiyo kutokana na ukosefu wa huduma kwa watu hao.

" Hivyo Busega mnatakiwa kuwekeza katika makundi hayo ili muweze kuondokana na hali ya ukosefu wa vifaa tiba katika wilaya yenu hii mpya, alisema Young .

Vifaa hivyo vitatumika katika hospital ya wilaya hiyo iliyopo kata ya Nyashimo wilaya humo ambayo bado inakabiliwa na uhaba wa vifaa kwa ajili ya wananchi wanaokwenda hapo kuweze kupata huduma za kutosha.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo la Busega Dr Raphael Chegeni ameipongeza serikali ya Korea Kusini kwa kutambua umuhimu wa jimbo lake hasa katika uhaba wa vifaa katika hospital hiyo ya Nyashimo.

" Hivyo nia yao walioonyesha ya kuwasaidia wanabusega ni njema na ni ya kuigwa kwa wadau wengine na hii ni kutokana na upya wa wilaya hiyo ya Busega, alisema chegeni

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni