Wilfried Zaha ametokea benchi na
kuisaidia Ivory Coast, kupata ushindi kwa kuifunga Sweden magoli 2-1
katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na Kombe la Mataifa ya Afrika.
Baada ya kutoswa na makocha Roy Hodgson na
Sam Allardyce, pamoja na Gareth Southgate, katika timu ya taifa ya
Uingereza Zaha ameamua kuichezea nchi yake aliyozaliwa ya Ivory
Coast.
Akicheza kwa mara ya kwanza na Ivory
Coast mchezaji huyo wa kimataifa aliingia dimbani baada ya mapumziko
Zaha, alitoa pande kwa Giovanni Sio aliyefunga goli la pili.
Wilfried Zaha akielekea kupiga krosi iliyozaa goli la ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni