Kocha Jose Mourinho amejiweka katika
nafasi ya kutwaa kikombe cha kwanza akiwa na Manchester United baada
ya jana kuifunga Hull City magaoli 2-0 katika nusu fainali ya kombe
la EFL.
Baada ya kuhangaika mno kujaribu
kuipenya ngome ya Hull, United wakiwa nyumbani walifanikiwa kufunga
goli la kwanza kupitia kwa Juan Mata akiunganisha mpira wa kichwa
uliopigwa na Henrikh Mkhitaryan.
Kipa wa Hull City, Eldin Jakupovic,
ambaye aliokoa michomo kadhaa ya wachezaji wa Manchester United,
alijikuta akifungwa goli la pili na Marouane Fellaini aliyetokea
benchi akiunganisha kwa kichwa krosi ya Matteo Darmian.
Juan Mata akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Marouane Fellaini akipiga kwa kichwa mpira na kufunga goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni