Timu ya Azam FC, kuanza rasmi
mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari
wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali za kiafya za
baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.
Wachezaji wa Azam FC waliokuwa
majeruhi ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’, Stephan Kingue
waliopata majeraha ya misuli ya paja kwenye mchezo uliopita wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, ambao matajiri hao
walishinda bao 1-0 lililofungwa na Bocco.
Wengine wanaouguza majeraha, ambao
waliukosa mchezo huo ni kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kipa
Mwadini Ally (nyama za paja) na beki Shomari Kapombe, ambaye ni
mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea vema.
Akizungumza na mtandao rasmi wa
klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya jana, Mwankemwa
alisema kuwa Bocco na Kingue watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki
mbili tokea jana, huku Sure Boy akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo
na Mwadini akipumzishwa kwa siku tatu kuanzia jana.
“Bocco hali yake inaonekana
kuimarika vizuri tokea alipopata majeraha hayo ya kuchana msuli wa
nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa upande wake naye amechana msuli
wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki
mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi mepesi baada ya wiki
moja,” alisema.
Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema
hali za wachezaji wengine ziko vizuri kabisa kuendelea na
mikikimikiki ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi pamoja na
michuano mingine.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni