.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Januari 2017

OLIVIER GIROUD KAMA 'MKHI' WA MAN U ATUMBUKIZA GOLI TAMU

Goli tamu la Olivier Giroud alilolifunga kwa mpira wa kisigino kwa nyuma limechochea ushindi wa Arsenal wa magoli 2-0 dhidi ya Crystal Palace na kukwea hadi katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi.

Mfaransa Giroud alilazimika kujaribu bahati kwa kupiga mpira kwa mtindo wa shuti la Nge baada ya pande la Alexis Sanchez kupitia nyuma yake.

Arsenal ilipata goli lake la pili kupitia kwa Alex Iwobi aliyefunga kwa mpira wa kichwa, kabla ya Palace kupoteza nafasi nzuri ya kufunga iliyookolewa na kipa Petr Cech.
                          Olivier Giroud akifunga goli la kwanza la Arsenal kwa shuti la Nge
                                                         Alex Iwobi akifunga goli kwa mpira wa kichwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni