.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 3 Januari 2017

POLISI WAKUTA WAHAMIAJI WAMEFICHWA KWENYE DASHBOARD NA KWENYE SANDUKU

Polisi nchini Hispania inawashikilia raia wawili wa Morocco ambao walikuwa wakijaribu kuwaingiza kwa kificho wahamiaji wawili wakiwa amefichwa kwenye gari na mwingine kwenye sanduku.

Wakati polisi wakikagua gari siku ya Jumatatu, mmoja wa wahamiaji hao alikutwa amefichwa kwenye dashboard na mwingine akakutwa amewekwa eneo la nyuma la kiti.

Wahamiaji hao haramu mmoja mwanaume na mwingine wa kike ambao inadhaniwa kuwa ni raia wa Ghana, wamepatiwa huduma ya kwanza kutokana na kuishiwa pumzi kwa kukosa hewa ya kuvuta.

Katika tukio lingine kijana mdogo wa kiume alikutwa akiwa amefichwa ndani ya sanduku la mwanamke akivushwa mpakani kimagendo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni