.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 29 Januari 2017

RAIS DONALD TRUMP APIGA SIMU NA KUONGEA NA VIONGOZI SABA WA DUNIA

Rais Donald Trump amepiga simu kadhaa na kufanya mazungumzo na viongozi wa dunia jana akiwemo rais Vladimir Putin wa Urusi.

Urusi imesema pande zote mbili zimeafikiana kupambana na ugaidi wa kimataifa ikiwamo kundi la Dola ya Kiislam (IS) pamoja na makundi mengine ya kigaidi ya Syria.

Ikulu ya Marekani imesema mazungumzo hayo yalikuwa ni ya mwanzo mzuri wa kuimarisha mahusiano yaliyoanza kuyumba.

Rais Trump pia ameongea na viongozi wa mataifa ya Japan, Ujerumani, Ufaransa na Australia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni