Theo Walcott amefunga magoli matatu
'hat-trick' huku Danny Welbeck akirejea kwa kishindo dimbani tangu
Mei 2016 kwa kufunga magoli mawili wakati Arsenal ikiichakaza
Southampton kwa magoli 5-0 katika mchezo wa kombe la FA.
Katika mchezo ambao ulichezwa huku
timu zote mbili zikiwa zimebadilisha karibu wachezaji wake wengi,
kikosi cha Claude Puel kilijikuta kikifundishwa kusakata soka, baada
ya kufanikiwa kutinga fainali ya kombe la EFL dhidi ya Liverpool siku
ya jumatano.
Welback, aliyerejea dimbani baada ya
kuwa majeruhi kwa muda mrefu akiuguza goti baada ya kufanyiwa
upasuaji, aliifanya Arsenal iongoze kwa kupachika magoli mawili
mazuri ndani ya dakika 22 za kwanza na kumtengenezea Walcott goli la
tatu.
Arsenal ikicheza huku kocha Arsene
Wenger akifuatilia mpira jukwaani baada ya kufungiwa kukaa benchi
mechi nne, iliongeza machungu kwa Southampton baada ya mapumziko
baada ya kumuingiza Alexis Sanchez na kumsaidia Walcott kufunga
magoli mengine mawili.
Danny Welbeck akiwa amepiga mpira uliojaa wavuni na kufunga goli
Mpira uliopigwa na Theo Walcott ukiwa umejaa wavuni



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni