.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 5 Januari 2017

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI NNE ZAKUSANYWA NA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA ARUSHA KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI

Na Woinde Shizza,Arusha

Jumla ya shilingi TSH 4,708,680,000 zimekusanya na jeshi la polisi mkoa wa Arusha kikosi cha usalama barabarani kutokana na faini zilizolipwa na watumiaji wa vyombo vya moto kwa kipindi cha January 2016 hadi December 2016 hiii ikiwa ni ongezeko kubwa tofauti na miaka iliopita

Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa ya hali ya usalama kwa kipindi chote cha mwaka 2016 kuanzia January hadi December ambapo alisema kuwa kwa upande wa ukusanyaji wa notification fedha zimeongezeka kwa kiasi kikubwa .

Alisema kuwa tozo hizo za noitficationi katika kipindi cha mwaka 2016 ziliongezeka hadik kufikia TSH 4,708,680,000/= tofauti na mwaka 2015 ambapo jumla ya TSH3,227,640,00/= zilikusanywa kwa hivyo kutokana na takwimu hizi kikosi cha usalama barabarani kimekusanya ongezeko la zaidi ya shilingi TSH 1,481,040,000/=.

“fedha hizi zimeongezeka kutokana na makosa mbalimbali yanayofanywa na madereva mbalimbali wa vyombo vya moto kwa kujua wanavunja sheria ,na wengine wakiwa wanafanya kwa kutokujua sasa sisi kama jeshi la polisi tunatumia njia ya kuwaonya kwa kuwatoza faini ili waweze kujirekebisha kwa haraka kwa sababu tusipo fanya hivyo na kuwaonya bila kuwapiga faini watakuwa wanarudia makosa kila siku ,na pia ongezeko hilo limetokana na kuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaotumia vyombo vya moto ,mfano ukiangalia magari mjini uwezi kufananisha magari yaliyokuwepo mwaka jana na mwaka huu mwaka huu yameongezeka kwa kasi na hata pikipiki pia ni hivyo hivyo”alisema Mkumbo9.

Aidha laisema kuwa hali ya usalama barabarani kwa mwaka 2016 ilizidi kuimarika maradufu tofauti na mwaka 2015 kwani twakimu zinaonyesha mwaka 215 kulikuwa na jumla za ajali kubwa 85 fofauti na mwaka 2016 jumla ya ajali kubwa ni 70 ambapo kuna punguza ya zaidi ya ajali 15, alifafanua kuwa kati ya ajali hizo za vifo zilikuwa 49 kwa mwka 2015 ambapo kwa mwaka 2016 zilipungua na kufikia ajali za vifo 44 pungufu ya makosa tano huku watu waliofariki kutokana na ajali hizo 2015 walikuwa 58 na mwaka 2016 walkuwa watu 55 tu.

Mkumbo alisema kuwa katika mwaka katika kipindi chote cha mwaka jana hali ya usalama katika mkoa wa arusha inazidi kuimarika ambapo takwimu za kihalifu zimezidi kupungua kwa makosa 383 ambapo kwa mwaka 2015 kulikuwa na makosa 2,979 yaliyoripotiwa kimkoa kwa kipindi hicho cha mwezi January adi December na hii ni tofauti ya ya makosa yaliyoripotiwa kwa mwaka 2016 kwa mwezi January hadi December ambapo makosa yaliyoripotiwa yalikuwa 2596 ,mafanikio haya ya upungufu ya makosa ya kialifu 383 ni sawa na asilimia 6.8% nah ii imetokana na juhudi za askari ,ushirikiano wa vyombo vingine vya usalama ,wadau pamoja na wananchi ambao walikuwa wanasiaidia uhalifu

“pia makosa makubwa ya jinai nayo yamepungua kwa asilimia kubwa ambapo makosa ya mauaji kwa mwaka 2015 yalikuwa 77 tofauti na makasa 64 yaliyotokea mwaka 2016 ikiwa ni pungufu ya mkosa 13 huku makosa ya kubaka kwa mwaka 2015 yakiwa ni 170 tofauti na mwaka 2016 ambapo kulikuwa na makosa 142 pungufu ya makosa 28”alibainisha mkumbo

Aidha kamanda alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 makosa ya kulawiti yalikuwa 48ambapo kwa kipindi cha mwaka 2016 makosa hay9 yalipungua hadi kufikia 41 hivyo kulikuwa na upungufu wa makosa saba ,alisema kuwa kwa upande wa makosa ya kuibiwa watoto yaliongezeka kwani kwa mwaka 2015 watoto 4 waliibiwa na mwaka 2016 watoto sita walibiwa lakini pia jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kuwashikilia baadhi ya wauguzi na kuwafikisha mahakamani kutokana na kufanya uzembe kazini.

Mkumbo alimalizia kwa kuwashukuru wananchi wa mkoa wa arusha kwa kuwapa ushiirkianao aliwasihi kutoa ushirikiano zaidi kwa jeshi hilo ili kuweza kutokomeza uhalifu kabisa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni