Mpira wa adhabu uliopigwa na Alain
Traore katika dakika za mwisho umeisaidia Burkina Fasso kuifunga
Ghana na kutwaa nafasi ya tatu ya michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika.
Kutoka umbali wa yadi 18, Traore
aliachia shuti kali la mguu wa kushoto lililojaa kwenye kona ya juu
ya goli na kutinga wavuni katika dakika ya 89.
Matokeo hayo yameifanya Ghana iishie
katika nafasi ya nne kwa mara ya tatu katika michuano hiyo, huku
kocha wake Avram Grant hatma yake ikiwa mashakani.
Jordan Ayew, Edward Agyemang Badu na
Bernard Tekpetey wote walikosa nafasi za kuifungia Ghana katika
mchezo huo.
Kocha wa Ghana Avram Grant akiwa mwenye mawazo tele baada ya kushindwa kutwaa nafasi ya tatu Afcon
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni