Mshambuliaji Romelu Lukaku amefunga
magoli manne kwa jitihada zake binafsi wakati Everton ikiibuka na
ushindi wa magoli 6-3 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Goodison
Park.
Lukaku alifunga goli la kwanza kwa
mpira wa kuzungusha baada ya sekunde 30 tu na kuweka rekodi sawa na
mchezaji wa Chelsea, Pedro aliyefunga ndani ya sekunde kama hizo
katika mchezo dhidi ya Manchester United.
Lukaku alimtenegezea nafasi James
McCarthy na kufunga goli la pili, kisha yeye akaongeza la tatu
kupitia pasi ya nyuma iliyopigwa kimakosa na Simon Francis na
kumpatia nafasi Lukaku ya kufanya matokeo kuwa 3-0 katika kipindi cha
kwanza.
Romelu Lukaku akifunga goli la kwanza ndani ya sekunde 30 tu za mchezo
Mshambuliaji Romelu Lukaku akifunga goli la tatu la Everton
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni