Watumishi wa Mahakama wilayani Magu wakiandamana na bango lenye ujumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria
Na Shushu MAGU
Na Shushu MAGU
HAKIMU mfawidhi wa wilaya ya Magu
mkoani mwanza Edmund Kente ametoa agizo kwa mahakimu na watumishi
wote wa idara za mahakama kuhakikisha wanawashughulikia wananchi kwa
uhakika na ipasavyo.
Wito huo ameutoa katika siku ya
maadhimisho ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahaka
ya wilaya ya magu chini ya kauli mbiu iliyosema kuwa Umuhimu wa
utoaji wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Kente alitumia wito huo kuwataka
mahakimu wote wa mahakama za mwanzo kuweza kubadilika na kufanya kazi
kwa weredi ili kuleta ufanisi mkubwa katika kazi zao za kuwahudumia
wananchi wa hali ya kawaida kwa kuwawezesha kupata haki zao za
msingi.
Aliongeza kuwa wananchi
wanapokimbilia mahakani lengo lao ni kupata haki sitahiki ili waweze
kuepukana na hicho kilichokuwa kikiwasumbua katika kutambua haki zao
lakini hali imekuwa sivyo na matarajio yao nah ii ni kutokana na
mahakimu wengi kutokufanya kzi kwa weredi.
“Nimeletewa malalamiko mengi na
wananchi juu ya kuzungushwa kwa kesi zao na mahakimu bila kuwepo kwa
sababu za msingi na kuweza kuyatolea maamuzi magumu kwa baadhi ya
mahakimu wanaokuwa na tabia za kuwazungusha wananchi Alisema”.
Aidha hakimu huyo mfawidhi akiongeza
kuwa siku mbili nyuma waliweza kufanya ziara akiwa na watumishi wote
wa idara ya mahakama katika gereza la magu ili kuwajulia hali
wafungwa na kuwapatia zawadi mbalimbali kwa lengo la kutojenga uadui
kati yao na vyombo vya haki.
Pia aliongeza kuwa jeshi la polisi
na mahakama ni vyombo vinavyotegemewa katika kutenda haki kwa
wananchi lakini wengi imekuwa sivyo nah ii ni kutokana na wachache
kutozingatia maadili ya kazi zao.
Kwa upande wake hakimu wa Mahakam ya
mwanzo wilaya ya magu Reuben Muganyizi amempongeza hakimu kente kwa
utendaji wake wa kazi katika wilaya hiyo na kusema kuwa ni mfano wa
kuigwa katika jamii yetu.
Aidha ametumia muda huo kutoa
ushauri kwa mahakimu wenzake kwa kuiga tabia za kiongozi wao ambaye
amekuwa akitetea wananchi wa chini kwa kuwasiadia sheria mbalimbali
zikiwemo za ardhi na nyingine kibao kwa lengo la kuwaweka sawa katika
kutambua haki za msingi.
Muganyizi aliongeza kuwa si vyema na
wala si sahihi kuwaweka wananchi mahakamani kwa muda mrefu bila
kuwapatia huduma wanazohitaji kupata toka kwetu wanasheria ambao tupo
kwa ajili ya kuwsaidia wananchi.
Peter Msanja ni mchungaji mstaafu wa
kanisa la Mitume ya Yehova alisema Mahakam ni chombo cha kutoa haki
katika jamii lakini leo imekuwa ndio chombo cha upotoshaji katika
jamii isiyojua sheria lakini tangu tumpate hakimu kente mambo
yamekuwa tofauti na awali.
Mchunga huyo aliongeza kuwa hakimu
mfawidhi anafanya kazi kwa weredi na kwa haki ndio maana watu wengi
uenda kumuona yeye ili aweze kuwahudumia katika kutatua kero zao
pasipo upendeleo wa aina yeyote ile.
“Rushwa upofusha hivyo watu
wasitumie kitu ambacho hata kwenye vitabu vya mungu vimekataliwa kwa
makusudi ya kusongesha taifa mbele katika maendeleo”
MWISHO
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni