Alexis Sanchez amefunga mara mbili
wakati Arsenal inayofukuzi ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiifunga
Hull City iliyo katika hatihati ya kushuka daraja, magoli 2-0.
Katika mchezo huo wenyeji Arsenal
walikuwa katika ubora wao na Sanchez aliandika goli lao la kwanza
katika dakika ya 34 ya mchezo.
Sanchez alifunga goli la pili katika
dakika za majeruhi baada ya kuzawadiwa penati kufuatia Sam Clucas
kutolewa nje kwa kuushika mpira wa kichwa uliopingwa na Lucas Perez.
Alexis Sanchez akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza
Sam Clucas akipewa kadi nyekundu kwa kuushika mpira na kuifanya Arsenal kupewa penati iliyofungwa na Sanchez
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni