.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 22 Februari 2017

ATLETICO MADRID YAANZA VYEMA UGENINI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Timu ya Atletico Madrid imefunga magoli manne ya ugenini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 dhidi ya Bayer Leverkusen katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya magoli 4-2.

Saul Niguez aliwapatia wageni goli la kwanza kwa shuti la kuzungusha na kisha Antoine Griezmann kuongeza goli la pili kutokana na pasi ya Kevin Gameiro baada ya uzembe wa beki wa Leverkusen, Omer Toprak.

Karim Bellarabi alichomoa goli moja kwa Leverkusen, lakini mkwaju wa penati wa Gameiro ukaongeza goli la tatu. Stefan Savic alijifunga na kuipatia Leverkusen goli la pili hata hivyo Fernando Torres aliyetokea benchi akafunga goli la nne.
                        Karim Bellarabi wa Leverkusen akifunga goli katika kipindi cha pili
                         Mshambuliaji Fernando Torres akifunga goli la nne katika mchezo huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni