Manchester City imetokea nyuma mara
mbili na kupata faida ya magoli mawili katika mchezo wa Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 5-3 dhidi ya
Monaco katika mchezo uliopigwa katika dimba la Etihad.
Katika mchezo huo Raheem Sterling
aliipatia Manchester City goli kufuatia kazi nzuri ya Leroy Sane
lakini Monaco wakajibu mapigo kupitia kwa Radamel Falcao na kuongeza
goli la pili lililofungwa na Kylian Mbappe.
Falcao alishuhudia penati yake
ikiokolewa na kipa Willy Caballero dakika chache tu katika kipindi
cha pili kabla ya makosa ya kipa wa Monaco, Danijel Subasic, kumpatia
nafasi ya kufunga goli Sergio Aguero.
Raia wa Colombian Falcao, ambaye kwa
sasa amerejea kwenye kiwango chake baada ya kushindwa kufanya vyema
akicheza kwa mkopo Manchester United na Chelsea, alifunga vyema kwa
mpira wa kunyanyua juu uliomshinda kipa Caballero.
Aguero ambaye anahisi alinyimwa
penati katika kipindi cha kwanza, alisawazisha kwa kufunga goli kabla
ya John Jones kuongeza goli la na kisha mchezaji bora katika mechi
hiyo Sane akafunga goli la tano.
Raheem Sterling akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Radamel Falcao akifunga goli la ufundi la kuubetua mpira kwa juu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni