Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa
Balozi Seif Ali Iddi akilifungua Kongamano ya maadhimisho ya kutimia
Miaka 40 ya CCM kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Magharibi
Unguja Kichama hapo Ukumbi wa Meli Nne Saccos.
Viongozi wa Juu wa CCM wakifuatilia
hotuba ya Mgeni rasmi Balozi Seif ambae hayupo Pichani, ambapo wa
kwanza kutoka Kushoto ni Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. Shamsi Vuai
Nahodha, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Nd. Yussuf Mohamed Yussuf.
Mke wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Taifa Balozi Seif , Mama Asha Suleiman Iddi kati kati akiwa shuhuda
wa Kongamo hilo la maadhimisho ya kutimia miaka 40 ya CCM, wa kwanza
kutoka Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mjini ambae
pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud na
wa kwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani Nd. Ali
Shunda.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa
CCM Mkoa Magharibi Unguja waliohudhuria Kongamano la kutathmini na
kujadili miaka 40 ya CCM.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa
CCM Mkoa Magharibi Unguja waliohudhuria Kongamano la kutathmini na
kujadili miaka 40 ya CCM.
Na. Othman Khamis Ame
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi alisema
wakati umefika kwa Viongozi na Wanachama wa CCM kuanzia ngazi ya
chini ya Tawi kujenga utamaduni wa kufanya tathmini ya ratiba ya
shughuli zao za kila siku za Chama hicho
kwa lengo la kuongeza nguvu pamoja
na uhai wa Chama.
Hata hivyo alisema tathmini hizoili
ziweze kuleta tija kwa CCM ni lazima zifanywe na Wataalamu waliomo
ndani ya Chama hicho au hata wa kuazima kutoka nje kufanya tathmini
hiyo Kitaalamu.
Akizungumza katika maadhimisho ya
Miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM katika Mkoa wa Magharibi Unguja Kichama
hapo katika Ukumbi wa Saccos Meli Nne Fuoni Balozi Seif Ali Iddi
ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba
tathmini isiyofuata taaluma haitakuwa na
maana yoyote bali ni kupoteza muda
na rasilmali za Chama.
Alisema Tathmini nzuri ni ile
inayowashirikisha Wanachama wa matabaka yote wakiwemo Wazee,
Vijana,Wanawake, Wanaume, Viongozi na hata wanachama wa kawaida
ikizingatia matokeo ya aina moja hata kama itafanywa na watu tofauti
wasiojuwana.
Balozi Seif alisema kwamba tathmini
iliyofanywa kwa misingi ya uadilifu na uaminifu mara nyingi husaidia
kuwabaini watu waliokuwa vikwazo vya maendeleo ndani ya Chama hicho
jambo ambalo lilichangia kuviza utendaji makini wa Chama.
Akizungumzia mabadiliko na Tathmini
masuala yanayokwenda sambamba katika utekelezaji wake alisema
wanachama wasiposhuhudia mabadiliko baada ya mikutano ya kutathmini
changamoto ndani ya kipindi cha miaka 40 ya CCM wanaweza kuvunjika
moyo.
Balozi Seif Ali Iddi alielezea
faraja yake kutokana na mafanikio makubwa ndani ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM
ambapo wanachama na Viongozi watakuwa na fursa za kuzieleza
changamoto zitakazojitokeza katika mapendekezo yao
kwenye utekelezaji wa ilani hiyo.
Balozi Seif ambae pia ni Mlezi wa
Mkoa huo wa Magharibi Unguja Kichama alitoa wito kwa wanachama wote
wa Chama cha Mapinduzi kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali
mbali za Uongozi ndani ya chama hicho wakati muda halisi wa kufanya
hivyo pale utakapowadia.
Akigusia tabia ya makundi ya baadhi
ya wanachama wa CCM yaliyoanza kuibuka yakijiandaa na uchaguzi Mkuu
wa 2020 Balozi Seif alionya kuachwa mara moja kasumba hiyo
itakayovuruga utendaji wa Seriali zilizopo madarakani wakati huu.
Balozi Seif alisema yapo makundi
yanayotajwa kuongozwa na baadhi ya Viongozi ambayo hayaleti sura
nzuri na kuendeleza tabia hiyo ni kukaribisha chuki za wenyewe kwa
wenyewe ndani ya chama.
Alisisitiza kwamba Viongozi na
Wanachama lazima wafikie wakati wakuaminiana na kuacha kasumba
zitakazokwamisha ushirikiano pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na
maelewano.
Balozi Seif alipendekeza wazi
kwamba wale wanachama na Viongozi wanaoonekana kuwa na sura mbili
katika mfumo wa utendaji kazi wao lazima waanze kuwekwa pembeni
kabisa.
Akitoa Taarifa ya Mkutano huo Mkuu
Maalum wa Mkoa Magharibi Unguja Kichama wa kongamano la kutathmini
miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM Katibu wa CCM wa Mkoa huo Bibi Aziza
Ramdhan Mapuri alisema maadhimisho hayo yameanza na shughuli za usafi
wa maingira katika maeneo tofauti ya Mkoa huo.
Bibi Aziza alisema harakati hizo
zilizoanza karibu wiki moja iliyopita ia zikatoa fursa kwa Viongozi
wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya mbili zilizomo ndani ya Mkoa huo
kufanya mikutano ya kutathmini Historia ya CCM Tokea ilipozaliwa
mwaka 1977 kwenye uwanja wa Amani Mjini
Zanzibar.
Katibu huyo wa CCM Mkoa Magharibi
Unguja Kichana alitumia nafasi ya Mkutano huo kuwanasihi Wajumbe wa
Mkutano huo, Viongozi wengine na Wanachama wa CCM kuwachagua
Viongozi wenye uzalendo uliotukuka wakati utakapowadia wa kufanya
chaguzi ndani ya Chama hicho Kikongwe.
Alisema hatua ya kuwachagua Viongozi
wazalendo ndio njia sahihi itakayowa9a uwezo wale watakaochaguliwa
kuwa na nguvu za kutekeleza wajibu wao bila ya kuogopa katika
uatekelezaji wa Ilani na Sera za Chama cha Mapinduzi.
Akimkaribisha mgeni rasmi kulifungua
Kongamano hilo la Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Magharibi
Unguja Kichama Mwenyekiti wa Mkoa huo Nd. Yussuf Mohamed Yussuf
alisema mfumo wa Sera na Ilani ya CCM unawezesha Chama hicho kuwa na
matarajio ya kuongoza Dola kwa miaka mingi ijayo.
Nd. Yussuf alisema mfano wa hayo ni
pale inapotokezea chaguzi ndogo za Jimbo la Serikali za Miataa jinsi
CCM inavyoibuka kidedea na kuonyhesha ishara ya kuendelea kuungwa
mkono na Wananchi walio wengi katika maeneo mbali mbali Nchini
Tanzania.
Mkutano Mkuu huo Maalum wa CCM Mkoa
wa Magharibi Unguja Kichama ulijumuisha mada mbili muhimu zitakazotoa
fursa kwa wajumbe wa Mkutano huo kuzijadili na hatiame kutoa
mapendekezo yao yatakayowasilishwa katika Uongozi wa juu wa chama
hicho kwa kufanyiwa kazi.
Mada hizo ni pamoja na Historia ya
CCM, mafanikio ya miaka 40 ya CCM, changamoto na sababu
zake,mapendekezo ya namna ya kuzishughulikia changamoto hizo.
Mada nyengine ni mafanikio ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 iliyopata ridhaa ya
wananchi walio wengi katika kuongoza Dola.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
5/2/2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni