Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijabe (Mb), akizungunza wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu
ugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta
Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private
Equity Project), mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa pili kulia) akiandika mambo mawili
matatu yaliyojiri wakati wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta
Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi
ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC
(Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), akihutubia washiriki wa semina
iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu
zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na
Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and
Private Equity Project), mjini Dodoma, ambapo waziri huyo ameitaka
sekta binafsi kuwezesha upatikanaji wa Zaidi ya shilingi Trilioni 48
ili kusaidia ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Maendeleo.
Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
KIASI cha Shlilingi Trilioni 48
kinahitajika kutoka Sekta Binafsi ili kufanikisha ujenzi wa miradi
mikubwa ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa
unaotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi mwaka
2020/2021
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango, amesema hayo mjini Dodoma wakati akifunga semina ya
siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPS
iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya
Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital
and Private Equity Project)
"Imekadiriwa kuwa mahitaji ya
fedha ya mpango huo ni takriban shilingi Trilioni 107, kati ya hizo
shilingi Trilioni 59, sawa na asilimia 55, zitatokana na mapato ya
Serikali na shiilingi Trilioni 48, sawa na asilimia 45 zitatokana na
vyanzo vya Sekta Binafsi.
Amesisitiza umuhimu wa Sekta Binafsi
kuwekeza zaidi kwenye kilimo na viwanda vitakavyosaidia kuongeza
thamani ya mazao ya wakulima ili waweze kunufaika kiuchumi na
kuendeleza nchi kwa ujumla
Dkt. Mpango, ameahidi kuwa Serikali
iko tayari kuhakikisha kuwa vitendea kazi muhimu vya utekelezaji wa
mradi huo vinapatikana ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya
ubia ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es
salaam kwenda Chalinze.
mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni