Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda
akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea banda ya maonyesho ya
Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global Education Link juzi.
Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje, Global
Education Link tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo (mwenye shati jeupe).
Kushoto ni Balozi wa India Sandeep Arya. Picha na mpiga picha wetu
Meneja wa GEL Dodoma, Hemed
Mlapakolo akizungumza jambo kwenye maonyesho ya biashara
Na Mwandishi wetu, Dodoma
KUTOKANA na Tanzania kujikita
kufufua uchumi katika sekta ya viwanda vya kati, Balozi wa India
nchini, Sandeep Arya, ameihakikishia Tanzania kuisapoti kwenye suala
la elimu kwa lengo la kuinua uchumi.
Akizungumza wakati akizindua
maonyesho ya biashara yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara,
Kilimo na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoani Dodoma kwa kushirikiana na
kampuni ya Global Education Link ya Tanzania juzi (jana), Balozi Arya
alisema kukua kwa kasi uchumi wa India, kulitokana na kuwapo vyuo
vingi vya elimu vyenye vifaa vizuri vya kufunduishia nchini humo.
“Kiwango cha elimu kinachotolewa
India ni cha hali ya juu kutokana na upatikanaji wa vifaa vya kutosha
vya kufundishia na kujifunzia, jambo linalowahakikishia wahitimu
kutoka vyuo mbalimbali kupata kazi kwa urahisi,” alisema Arya na
kuwashauri wanaotaka kusoma nje kuwasiliana na Global Education Link
kwa vile wana ushirikiano wa karibu na ubalozi huo.
Alisema suala la utandawazi na
mahusiano baina ya nchi hiyo na nyingine katika kurahisisha
upatikanaji wa mahitaji muhimu, linachangia kuwakutanisha watu wa
aina mbalimbali kupata elimu kutokana na kuwapo na vifaa vilivyopo.
Balozi Arya aliwahakikishia
washiriki wa maonyesho hayo kuwa upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya
kufundishia nchini India, kumesaidia kutolewa kwa kiwango cha juu cha
elimu.
Aidha, alisema baadhi ya mashirika
makubwa duniani, viongozi wake walifanikiwa kusoma nchini India na
kupata elimu iliyo bora.
Ubalozi wa India umeanzisha
ushirikiano na GEL katika kuwasaidia Watanzania wanaotaka kusoma nje
ya nchi hasa baada ya ubalozi huo kujiridhisha na namna kampuni hiyo
ya uwakala wa vyuo vya nje inavyowafuatilia wanafunzi wake hata baada
ya kuwaunganisha na vyuo vya nje kujua maendeleo yao.
Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo
Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo aliwataka watanzania
kujiimarisha katika ujuzi akisema ndio msingi wa kila kitu.
Baadhi ya wanufaika wa elimu kupitia
Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL),
akiwamo Pelagia Mauma, alisema alifanikiwa kupata elimu bora nchini
India kupitia kampuni hiyo kwa gharama iliyo nafuu zaidi.
“Gharama za elimu katika vyuo vyua
India ni nafuu zaidi, hawa wenzetu hawaangalii ada bali
wanachoangalia ni vipi mtu atafanikisha kupata elimu iliyo bora,”
alisema Mauma.
Afisa Mtendaji wa TCCIA mkoa wa
Dodoma, Fred Azaria pamoja na kueleza shughuli za chama chake,
alisema wanalenga kupunguza umaskini kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma
baada ya kuandaa maonyesho ya vifaa vya shule na zana za kufundishia
kutoka India.
“Nawaomba Watanzania waweze
kutumia fursa iliyopo ya kupata elimu, huku wakiwaomba Watanzania
kutumia fursa hiyo kujipatia elimu nchini India,” alisema.
Nae Meneja wa GEL tawi la Dodoma,
Hemed Mlapakolo alisema sababu ya kushirikik maonyesho hayo ni kutoa
nafasi kwa Watanzania kuhusiana na namna gani mtu anaweza kufanya
uchaguzi sahihi wa kozi ya pale anapotaka kusoma nje ya nchi.
“Tumekuwa mawakala wa vyuo vya nje
kwa zaidi ya miaka kumi sasa, wengi wamekuwa wakipitia kwetu
kuunganishwa na vyuo vya nje, tumeona tuje hapa ili waweze kupata
ufahamu zaidi kuhusiana na uchaguzi wa vyuo vya nje na uchaguzi wa
masomo ya kusomea pia,” alisema Hemed.
Hemed alifafanua kuwa kumekuwa na
changamoto kubwa kwa Watanzania katika uchaguzi wa nini cha kusoma.
“Utakuta wengi wanachojua ni udaktari, lakini kwenye udaktari kuna
wa aina nyingi, kuna udaktari wa magonjwa ufahamu, udaktari wa meno
tu, udaktari wa mifupa na kadhalika, kazi yetu ni kutoa ushauri wa
aina hii. Tunafanya hivi ili kukumbushana kwa sababu kama wengi
watakuwa kwenye fani au utaalamu wa aina moja, maana yake ni kwamba
fani nyingine zitakosa wataalam au zitakuwa na wataalam wachache,”
alisema.
IMETOLEWA NA IDARA YA MAWASILIANO
GLOBAL EDUCATION LINK
DAR ES SALAAM
LEO TAREHE 5 FEB 2017
SIMU: 0712183282
www.gel.co.tz
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni