Mbrazil Gabriel Jesus amefunga mara
mbili, likiwemo goli la dakika za majeruhi na kuifanya Manchester
City kukwea hadi katika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Uingereza
baada ya kuifunga Swansea magoli 2-1.
Jesus alianza kuonyesha makali yake
mara moja katika dimba la nyumbani, akitumia kasi yake kuwazidi kasi
mabeki wa Swansea na kufunga goli kwa mpira uliompita kipa Lukasz
Fabianski.
Wenyeji walitawala kipindi cha
kwanza lakini wageni walitumia ukosefu umakini wa Manchester City
baada ya Gylfi Sigurdsson kuinasa krosi ya Luciano Narsingh na
kutumbukiza mpira wavuni.
Mbrazil Gabriel Jesus akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Mchezaji Gylfi Sigurdsson akifunga goli pekee la Swansea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni