Cameroon imetokea nyuma ikiwa
imefungwa goli moja na Misri na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 na
kutwaa ubingwa mara tano wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mchezaji aliyetokea benchi Vincent
Aboubakar alifunga goli la ushindi dakika mbili kabla ya mpira
kumalizika akiupaisha mpira juu ya beki Ali Gabr na kutikisa nyavu.
Alikuwa Nicolas Nkoulou
aliyeisawazishia goli Cameroon, baada ya kuruka juu na kufunga kwa
mpira wa kichwa.
Misri ilikuwa ya kwanza kupata goli
lililofungwa na Mohamed Elneny katika dakika ya 22 kwa shuti safi la
karibu ya goli.
Mohamed Elneny akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Vincent
Aboubakar akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni na kuipa ushindi Cameroon
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni