Cameroon itaivaa Misri katika
fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kupata magoli mawili
katika kipindi cha pili katika michezo wa nusu fainali dhidi ya
Ghana.
Pande zote mbili zilipata nafasi
nzuri za kutikisa nyavu lakini mambo yalikuwa magumu hadi pale
Michael Ngadeu-Ngadjui alipotikisa nyavu kwa mpira wa adhabu katika
dakika ya 72.
Ikiwa zimebakia sekunde tu kabla ya
mchezo kuisha Christian Bassogog alifunga goli la pili la ushindi kwa
shambulizi la kushtukiza.
Wachezaji wa Ghana wakionyesha kuchanganyikiwa baada ya kufungwa goli la kwanza
Kipa wa Ghana Brimah Razak akiuangalia mpira ukiingia wavuni na kuipatia Cameroon goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni