Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza
Chelsea wametinga robo fainali ya kombe la FA kwa ushindi wa magoli
2-0 dhidi ya Wolves katika dimba la Molineux.
Katika mchezo huo Wolves walianza
kwa kuleta kashikashi katika goli la Chelsea ambapo George Saville
nusura afunge goli lakini shuti lake likagonga mwamba.
Beki ya Chelsea iliendelea
kujaribiwa na Wolves, hadi pale Chelsea ilipocharuka na kufunga goli
la kwanza kupitia kwa Pedro na kisha Diego Costa kukamilisha ushindi.
Pedro akiwa ameupiga kwa kichwa mpira uliomshinda kipa na kufunga goli la kwanza
Mpira wa shuti uliopigwa na Diego Costa ukijaa wavuni na kufanya matokeo kuwa 2-0
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni