.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 26 Februari 2017

CHELSEA YAJIKITA KILELENI KWA TOFAUTI YA POINTI 11

Chelsea imeongeza uongozi wao katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 11 baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Swansea City katika dimba la Stamford Bridge.

Cesc Fabregas aliyetimiza michezo 300 ya ligi kuu alikuwa wa kwanza kufunga goli kwa kupenyeza mpira kati kati ya miguu ya Jack Cork na kujaa wavuni.

Wenyeji hawakushitushwa na kitendo cha Swansea kusawazisha goli hilo baada ya Fernando Llorente kuupiga kwa kichwa mpira adhabu uliopigwa na Gylfi Sigurdsson.

Fabregas aligonga mwamba kabla ya Pedro kufunga kwa shuti la mpira wa kuzungusha na kisha Diego Costa kukamilisha ushindi kwa kufunga goli la tatu.
                                                      Cesc Fabregas akifunga goli la kwanza la Chelsea 
                         Fernando Llorente akiwa ameupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli
                                         Mshambuliaji Diego Costa akifunga goli la tatu la Chelsea 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni