Timu ya Everton imeongeza rekodi yao
ya kutokufungwa kwa kushinda mchezo wao wa tisa mfululizo katika Ligi
Kuu ya Uingereza dhidi ya timu iliyomkiani ya Sunderland.
Licha ya ulinzi mkali wa beki ya
Sunderland, Idrissa Guaye alifunga goli lake la kwanza akiwa na
Everton akiunganisha krosi ya chini ya Seamus Coleman.
Sunderland iliongeza presha kwa
Everton kwa kutengeneza nafasi kadhaa huku shuti la Jermain Defoe
likigonga mwamba, kabla ya Romelu Lukaku kuongeza goli la pili.
Idrissa Guaye akijipinda kufunga goli la kwanza la Everton
Romelu Lukaku akibetua mpira na kufunga goli la pili la Everton
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni