Kocha wa Bayern Munich, Carlo
Ancelotti amesherehekea mechi ya 1,000 akiwa kama kocha wakati timu
yake ikiiaibisha Hamburg kwa magoli 8-0, huku Robert Lewandowski
akifunga hat-trick.
Hadi mapumziko Bayern ilikuwa
ikiongoza kwa magoli 3-0, yaliyofungwa na Arturo Vidal na Lewandowski
aliyefunga goli la pili kwa mkwaju wa penati kabla ya kufunga goli
lingine la tatu.
Mshambuliaji huyo raia wa Poland
alifunga goli lingine baada ya mapumziko, huku David Alaba na
Kingsley Coman wote wakifunga mara mbili, naye Arjen Robben
akakamilisha karamu kwa kufunga goli la nane.
Kwa matokeo hayo Bayern inaongoza
ligi hiyo kwa tofauti ya pointi tano ikifuatiwa na RB Leipzig katika
nafasi ya pili iliyoifunga Cologne magoli 3-1.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni