Rais Donald Trump amesema kuwa
hatohudhuria hafla ya Mlo wa Usiku na Ikulu iliyoandaliwa na Chama
cha Waandishi wa Habari wa Kujitegemea Aprili 29.
Hafla hiyo huwa inahudhuriwa na watu
mashuhuri, waandishi wa habari, wanasiasa na kwa kawaida rais wa
Marekani anakuwepo.
Hata hivyo rais Trump amesema
hatohudhuria hafla hiyo ikiwa ni siku moja tu kupita tangu Ikulu ya
Marekani kuvizuia vyombo kadhaa vya utangazaji na magazeti kuhudhuria
mikutano ya Ikulu.
Rais Trump amekuwa mara kwa mara
akielezea habari zinazomkosoa kama habari feki, na kuvishambulia
vyombo vinavyomkosoa.
Rais Donald Trump ametumia twitta kuelezea uamuzi wake huo
Donald Trump aliwahi kuhudhuria hafla hiyo, hii ilikuwa mwaka 2015
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni