Gari lililokuwa likiendeshwa kwenye
mkusanyiko wa watu katika paredi ya Mardi katika Mji wa New Orleans
Marekani limejeruhi watu 28, baadhi yao hali zao ni mbaya.
Gari hilo liliwagonga watu ambao
walikuwa wakiangali paredi ya Krewe of Endymion katika Wilaya ya
Mid-City jumamosi jioni.
Mtu mmoja anashikiliwa na polisi
akihisiwa kuwa alikuwa anaendesha gari akiwa amechoka, na polisi
wamesema tukio hilo si la kigaidi.
Dereva wa gari hilo aina ya pick-up
truck imeelezwa kuwa alikuwa hajitambui alichofanya wakati akikamatwa
na polisi.
Watu wakitoa huduma ya kwanza kwa mtoto aliyejeruhiwa
Majeruhi akikimbizwa kupandishwa kwenye gari la wagonjwa kuwahishwa hospitali
Polisi wakiwa wamemkamata dereva wa gari lililogonga watu na kujeruhi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni