Winga Shiza Ramadhani Kichuya
amemaliza ukame wa kutofumania nyavu na kuchagiza ushindi wa Simba
wa magoli 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi Kuu ya Tanzania
bara.
Kichuya sasa anaonekana kuwa na
kismati na Yanga, kwani katika mchezo uliopita aliisawazishia Simba
goli kwa mkwaju mzuri wa mpira wa kona uliojaa wavuni.
Lakini jana tena aliifanya Simba
ifikishe pointi 54 na kuongoza ligi, kwa kutengeneza goli la
kusawazisha na kisha baadaye akafunga goli bora kabisa la shuti la
mbali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni