Vinara Real Madrid wamepata kipigo
cha pili katika Ligi ya La Liga katika msimu huu baada ya kukubali
kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Valencia.
Mshambuliaji wa zamani wa West Ham,
Simone Zaza alikuwa wa kwanza kufunga goli kwa wenyeji na kisha
Fabian Orellana kuongeza goli la pili kabla ya Cristiano Ronaldo
kuchomoa moja.
Cristiano Ronaldo ambaye aliondoa
gundu la kutofunga kwa muda alikosa nafasi ya kuisaidia Real Madrid
kuambulia pointi moja baada ya mpira wake wa kichwa ulikosa kulenga
goli.
Cristiano Ronaldo akikimbia na mpira baada ya kufunga goli
Gareth Bale akiwa ameshika kiuno baada ya jahazi kuzama
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni