.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Februari 2017

JAMIE VARDY AFUNGA GOLI MUHIMU LICHA YA LEICESTER CITY KULALA

Jamie Vardy ametoa gundu la kutofunga goli kwa muda wakati Leicester City ikipata goli muhimu la ugenini na kuimarisha matumaini ya kutinga hatua ya nane bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kufunga magoli 2-1 dhidi ya Sevilla.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa amecheza mechi tisa bila kufunga goli na alikuwa mtu muhimu katika mchezo wa jana kwa kuonyesha uhai, ambapo alifunga goli hilo akiunganisha krosi ya Danny Drinkwater.

Goli hilo lilikuwa kati ya mashuti hatari mawili ambayo Leicester City ilifanya katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na wenyeji Sevilla walioongoza kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Pablo Sarabia kwa kichwa na shuti la karibu la Joaquin Correa.
                           Pablo Sarabia akiwa ameupiga mpira wa kichwa uandika goli la kwanza
                                 Mshambuliaji Jamie Vardy aifunga goli muhimu kwa Leicester City

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni