.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Februari 2017

MANCHESTER UNITED YATINGA KIULAINI HATUA YA 16 BORA LIGI YA UROPA

Manchester United imetinga kiulaini hatua ya 16 bora ya Ligi ya Uropa kwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Saint-Etienne lakini mfungaji Henrikh Mkhitaryan aliumia na anaweza kukosa mchezo wa fainali ya kombe la EFL jumapili.

Ikiwa inaongoza kwa ushindi wa 3-0 katika mchezo wa awali ambao Zlatan Ibrahimovic alifunga magoli matatu yaani hat-trick, United katika mchezo wa jana ilipata goli la mapema pale Mkhitaryan aliitumbukiza krosi iliyopigwa na Juan Mata.

Hata hivyo mchezaji huyo raia wa Armenia alitoka nje ya uwanja muda mfupi tu baada ya kupata majeraha ya misuli ya paja, hali ambayo itaathiri mipango ya kocha Jose Mourinho katika kupanga kikosi kitakachoivaa Southampton jumapili katika dimba Wembley.
                                    Henrikh Mkhitaryan akifunga goli pekee katika mchezo huo
                           Eric Bailly akipewa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni