Mchezaji wa zamani wa Manchester
United Dwight York amesema alijikuta akijihisi kama mhalifu, pale
alipokatiliwa kuingia Marekani, siku ya jana.
Yorke, mwenye umri wa miaka 45,
amesema alizuiwa kuingia Marekani kutokana na paspoti yake kuwa na
mhuri wa Irani, jambo ambalo aliambiwa atalazimia kuomba viza kwanza.
Yorke alikuwa akisafiri kutokea Doha, Qatar kwenda Trinidad and Tobago, ambako ananyumba yake lakini
alizuiwa akiwa njiani kuingia Miami, Marekani.
Rais Donald Trump akionyesha agizo alilotea saini la kuzuia kuingia Marekani raia wa Mataifa saba ya Kiislam likiwemo taifa la Iran


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni