Watu wawili wamekufa na makumi
kuokolewa wakati kimbunga kikubwa kilichoambatana na mvua kikileta
maafa kusini mwa California nchini Marekani.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 55
amekufa hospitalini baada ya kupigwa na shoti ya waya wa umeme
ulioangukiwa na mti Jijini Los Angeles.
Mwanaume mwingine amekufa maji huko
Victorville wakati gari lake aina ya Mercedes liliposombwa na
kupinduliwa na maji.
Askari wa kikosi cha zimamoto wakimuokoa mwanamke mmoja ambaye gari lake limezingirwa na maji
Lori likiwa limepinduka chini baada ya kusukumwa na upepo mkali wa kimbunga
Mmoja wa abiria akipanda basi katika kituo ambacho kilikuwa kimefurika maji ya mvua
Waokoaji wakiwa wamekata sehemu ya mti mkubwa ulioangukia gari na kufunga barabara





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni