Mchezaji Gabriel Jesus amefunga goli
lake la kwanza akiwa na Manchester City wakati wakiichakaza West Ham
4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza katika dimba la London.
Manchester City, ambao walimuacha
mshambuliaji wa Sergio Aguero na kipa Claudio Bravo akiwa benchi
walipata goli la kuongoza kupitia kwa Kevin de Bruyne baada ya
kugongeana vyema na Jesus.
Dakika nne baadaye Leroy Sane
aliwapita mabeki wawili na krosi yake iliyobabatizwa ikamkuta David
Silva na kufunga goli. Raheeem Sterling alimtengenezea goli Jesus na
Yaya Toure akafunga goli la nne kwa mkwaju wa penati katika kipindi
cha pili.
Kevin de Bruyne akifunga goli la kwanza la Manchester City
Yaya Toure akipiga mkwaju wa penati na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni