Misri imefikisha rekodi ya kutinga
mara tisa katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ikiwafunga
Burkina Faso magoli 4-3 kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kutoka
sare ya goli 1-1 na Burkina Faso.
Kipa mkongwe Essam El Hadary
amedhihirisha kuwa ni shujaa wa Misri, kwa kuokoa penati iliyopigwa
na Bertrand Traore na kuisaidia kupata ushindi.
Katika dakika za kawaida za mchezo
huo Mohamed Salah aliifungia Misri goli la kwanza kwa shuti zuri la
kuzungushwa lakini Burkina Faso wakasawazisha kupitia kwa Aristide
Bance.
Essam El Hadary akipangua mkwaju wa penati ya Bertrand Traore
Bertrand Traore akionekana mwenye mawazo baada ya kukosa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni