.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 22 Februari 2017

KASEJA MCHEZAJI BORA WA JANUARI LIGI KUU YA VODACOM

Golikipa wa timu ya Kagera Sugar, Juma Kaseja Juma amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Januari kwa msimu wa 2016/2017.

Kaseja aliwashinda wachezaji Mbaraka Abeid pia wa Kagera Sugar na Jamal S. Mtengeta wa Toto African.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/796-kaseja-mchezaji-bora-wa-januari-ligi-kuu-ya-vodacom

NAPE KUZINDUA MFUKO WA KUSAIDIA SERENGETI BOYS

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (Mb) kesho Februari 23, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.

Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa

Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/797-nape-kuzindua-mfuko-wa-kusaidia-serengeti-boys

MALINZI AZIPONGEZA SINGIDA UNITED, NJOMBE MJI

Mara baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuipongeza timu ya Lipuli ya Iringa, leo Jumanne Februari 21, mwaka huu kwa mara nyingine, Rais wa TFF Jamal Malinzi amezipongeza kwa mpigo, timu za Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe kwa kupanda daraja.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/794-malinzi-azipongeza-singida-united-njombe-mji

MKUTANO WA BARAZA KUU LA BODI YA LIGI FEBRUARI 26, 2017

Mkutano wa Tatu wa Baraza Kuu la Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) chini ya Mwenyekiti wake Bw. Hamad Yahya Juma utafanyika Jumapili, Februari 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Mkutano huo wa mwaka 2016 ambao utaanza saa 4 asubuhi ni wenyeviti wa klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom, na klabu zote za Ligi Daraja la Kwanza.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/795-mkutano-wa-baraza-kuu-la-bodi-ya-ligi-februari-26-2017

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni