Kocha Claudio Ranieri amefukuzwa
katika timu ya Leicester City huku mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu
ya Uingereza wakipambana kutoshuka daraja baada ya siku 298 kupita
tangu watwae ubingwa huo.
Leicester City imechukua uamuzi wa
kushangaza wa kumtimua kocha huyo jana usiku ikiwa ni miezi tisa tu
kupita tangu kocha huyo Muitaliano kuisaidia kutwaa ubingwa wa
Uingereza na kuweka historia ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya
kwanza.
Mapema mwezi huu wamiliki wa klabu
hiyo wa Thailand walionekana kumuunga mkono kocha Ranieri
wakisisitiza nafasi yake katika klabu hiyo ipo salama, na wao
wanamuunga mkono kuendelea kuinoa timu hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni