Kiwanja cha ndege cha Dodoma, sasa
kinauwezo wa kupokea ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 90, baada ya
kurefushwa kwa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kwa kilometa
2.5.
Ndege ya Shirika la ndege la
Tanzania (ATCL), leo ikitua kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma
ikitokea mkoani Kigoma.
Mizigo ya abiria wa ndege ya shirika
la ndege Tanzania (ATCL), ikiwa ndani ya gari la kampuni inayotoa
huduma ya mizigo ya National Aviation Services (NAS), kwenye Kiwanja
cha ndege cha Dodoma.
Mkuu wa Dodoma (kushoto) Mhe. Jordan
Rugimbana akielekea kupanda ya ATCL akiwa ni mmoja wa abiria akitokea
kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma na kuelekea Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Kulia ni Meneja wa kiwanja
hicho, Bw. Julius Mlungwana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan
Rugimbana (kulia) akiagana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma,
Bw. Julius Mlungwana kabla ya kupanda ndege ATCL, akielekea Jijini
Dar es Salaam, leo.
Wanafunzi wa kidato cha nne katika
shule ya sekondari ya Uwela ya kitongoji cha Kikuyu mkoani Dodoma
wakiwa katika ziara ya mafunzo kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma,
leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni