Jahazi la mabingwa watetezi wa Ligi
Kuu ya Uingereza, Leicester City, limeendelea kuzama baada ya kupokea
kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa Swansea.
Katika mchezo huo, Alfie Mawson,
aliifungia Swansea goli la kwanza na kisha baadaye, Martin Olsson,
kuipatia goli la pili.
Kwa kipigo hicho Leicester City wapo
pointi moja juu ya mstari wa kushuka daraja, huku ikiwa haijafunga
goli katika ligi hiyo mwaka huu.
Alfie Mawson akiachia shuti lililoandika goli la kwanza la Swansea
Kapteni wa Leicester City, Wes Morgan akiwa ameshika mpira hata hivyo haikutolewa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni