Lionel Messi amefunga goli la dakika
za mwisho wakati Barcelona ikiifunga Atletico Madrid magoli 2-1 na
kukwea kileleni mwa La Liga kwa muda tu.
Rafinha aliipatia Barcelona goli la
kuongoza baada ya Luis Suarez, ambaye jitihada zake zilishindwa kuzaa
matunda.
Diego Godin alisawazisha alipofunga
kwa mpira wa kichwa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Koke, hata
hivyo Messi alifunga goli la pili katika dakika ya 86.
Diego Godin akifunga goli la kusawazisha kwa mpira wa kichwa
Lionel Messi akiwa amempoteza mahesabu kipa wa Atletico Madrid na kufunga goli la ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni