Manchester United imeshinda kombe la
EFL Cup jana usiku baada ya kuifunga Southampton magoli 3-2 katika
dimba la Wembley.
Zlatan Ibrahimovic alifunga goli kwa
mpira wa adhabu ulioifanya Manchester United iongoze kabla ya Jesse
Lingard kuongeza la pili.
Muitaliano Manolo Gabbiadini
alifunga goli moja kabla ya mapumziko kabla ya kuongeza la pili
dakika dakika tatu baadaye na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Hata hivyo alikuwa Ibrahimovic
aliyejibainisha kuwa shuja wa Jose Mourinho baada ya kufunga goli la
tatu kwa mpira wa kichwa na kuipa ubingwa Manchester United.
Wachezaji wa Manchester United wakishangilia ubingwa wao wa kombe la EFL
Kocha Jose Mourinho akiwa amebeba kombe la EFL huku akipunga mkono
Shujaa wa mchezo wa jana Zlatan Ibrahimovic akiwa amebeba kombe la EFL
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni