Timu ya Manchester City imepanda
hadi katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza
baada ya kupambana na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya
Bournemouth katika dimba la Vitality.
Akiwa ameanzia benchi mshambuliaji
wa Manchester City, Sergio Aguero, aliingia katika dakika ya 14,
kufuatia kuumia kwa mshambuliaji anayemyima namba kwa hivi sasa
Mbrazili Gabriel Jesus.
Lakini alikuwa Raheem aliyeipatia
Manchester City goli la kwanza, baada ya kipa Artur Boruc kuokoa mara
mbili magoli, Tyrone Mings alijikuta akijifunga goli la pili kufuatia
shinikizo la lililochangiwa na Aguero.
Raheem Sterling akifunga goli baada ya kupokea pasi kutoka kwa David Silva
Mshambuliaji Gabriel Jesus akitolewa nje baada ya kuumia dakika ya 14 ya mchezo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni