Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisisitiza jambo wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel (kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakisikiliza maelezo mbalimbali katika Kongamano hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel akisisitiza umuhimu wa Viwanda nchini Tanzanai
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka (kulia) akiwa na Zacharia Kicharo Meneja wa TIB Development Bank Ltd Lake Zone wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu
Kutoka Kulia ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa Viwanda Mkoa wa Simiyu, Peter Bahini Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini (SNC) na Emmanuely Lupembe Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini (SNC wakifatilia kwa makini kongamano la uwekezaji Mkoani Simiyu
Meza kuu wakifatilia mjadala katika Kongamano la Jukwaa la Biashara Simiyu
Kwaya ya AIC Bariadi, Simiyu wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha ulipaji kodiKatikati ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa Viwanda Mkoa wa Simiyu akifuatilia kwa makini Kongamano
Wafanyakazi wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
Kutoka Kulia ni Mtafiti Mwandamizi (TSN) Bw Akim Joseph, Afisa masoko Mwandamizi (TSN) Goodluck Chuwa, Mwakilishi wa TSN Kanda ya ziiwa Patrice Simbachawene na Meneja wa Masoko na Mauzo wa TSN Bw Januarius MagangaMbunge wa Busega Mkoani Simiyu Mhe Raphael Chegeni akitoa salamu za shukrani kwa kufanikiwa kwa kongamano hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel (kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakiteta jambo wakati wa Kongamano
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka akiwasilisha MadaMhariri Mtendaji wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal akiendelea na kazi ya kuhabarisha kuhusu kongamano hilo
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw Richard Kayombo akielezea namna ya ukusanyaji Mapato
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wadau wawezeshaji wa Kongamano hilo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji Mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na Waimbaji wa Kwaya ya AIC Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki kuhabarisha kuhusu Kongamano hilo
Na Mathias Canal, Simiyu
Wafanyabiashara na wadau wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji wa biashara hususani katika kuwekeza kwenye viwanda kwani mipango mingi inayopangwa na serikali inatoa fursa zaidi kwa wawekezaji wa ndani ya nchi jambo ambalo litaifanya Tanzania kuondokana na umasikini kutokana na fursa zilizopo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu lililofanyika katika Ukumbi wa Parokia ya Mtakatifu John lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Rc Mtaka amesema kuwa Katika kuchochea na kuleta maendeleo kwa wananchi katika Mkoa wa Simiyu uongozi wa Mkoa huo una dhamira ya dhati kuwafanya wananchi wake kuingia katika ramani ya Mkoa unaotumainiwa nchini.
“Sisi viongozi kwa kushirikiana na wananchi tunapaswa kutumia Busara nyingi, Hekima na Utii ili kuimarisha utendaji katika maendeleo ya Mkoa kwa kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo pasina kutumia majungu ambayo yatadhoofisha maendeleo” Alisisitiza Mhe Mtaka
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel amewasihi wananachi ambao ni wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa wa Simiyu na wale wanaotaka kuwekeza Mkoani humo kufanya biashara na kuhakikisha wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria kwani wasipofanya hivyo biashara zao haziwezi kuwa na maendeleo kwani watakuwa wameenda kinyume na mamlaka ya Mungu inayoagiza kulipa kodi.
Prf Gabriel amebainisha hayo huku akihuisha na maneno yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu kwenye Kitabu cha Warumi 13:1-7 ambayo inaeleza vyema kwamba Mtu wa kodi apewe kodi na Mtu wa Ushuru apewe ushuru hivyo wafanyabiashara hao wanapaswa kutii mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Amesema Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia Mkuu wa Mkoa huo kuwa wanapaswa kuendelea zaidi kuwa wabunifu katika shughuli mbalimbali ili Simiyu iendelee kukua zaidi katika uwekezaji na maendeleo.
Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper inayochapisha magazeti ya Habari Leo, Daily News na Sport Leo Dkt Jim Yonazi amesema kuwa kampuni hiyo ya TSN imeamua kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ili kuufanya mkoa huo kuungana na Dunia katika kuakisi uwekezaji hususani katika sekta ya Viwanda.
Dkt Yonazi amesema kuwa kampuni ya TSN ina amini kuwa maendeleo ni habari hivyo kupitia Jukwaa hilo la Biashara katika Mkoa wa Simiyu watanzania na Dunia kwa ujumla itafahamu vyema juu ya umuhimu wa uwekezaji hivyo kupitia umoja na mshikamano kwa wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa huo utakuwa chachu ya mafanikio ya Tanzania nzima.
Hata hivyo amesema kuwa Mkutano huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya nguvu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo hata hivyo amewasihi wawekezaji na wadau wa Maendeleo kutumia nguvu hiyo kwa ajili ya biashara zao.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw Richard Kayombo ameelezea sababu za wawekezaji na wananchi kulipa kodi ambapo amesema kuwa njia pekee ya ambayo serikali inaweza kujipatia kipato chake kwa ajili ya kuwajengea wananchi Miundombinu bora, Kudumisha sekta ya Afya, Elimu na sekta zingine nyingi ni kukusanya kodi pekee.
Hata hivyo alisema kuwa zipo sekta ambazo kisheria zinapewa msamaha wa kutokulipa kodi ambapo ni pamoja na sekta ya Kilimo sambamba na sekta ya elimu na afya.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka amesema kuwa Bank hiyo ni maalumu kwa ajili ya shughuli za maendeleo na Biashara hivyo wajibu wake ni kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi hususani katika msaada wa kifedha.
Wadau wengine walioshiriki katika Jukwaa hilo la Biashara ni pamoja na TIB Development Bank, National Microfinance Bank (NMB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na TIB Development Bank Ltd.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni