Mfanyakazi mmoja wa shambani nchini
Kenya, amejiuwa baada ya muajiri wake kushindwa kumlipa malimbikizo
ya madai ya mishahara yake ya miaka miwili.
Mfanyakazi huyo, Nelson Anyamba,
mwenye miaka 38, amejiuwa kwa kujichoma choma kwa kisu baada ya
kutolipwa mshahara wake wa shilingi 5,000 ya Kenya kwa mwezi, kwa
muda wa miezi 24.
Mke wa marehemu, Phyllis Sariku,
amesema muajiri wa mumewe alikuwa anadaiwa kiasi hicho cha sh 120,000
za Kenya lakini alimlipa sh 5,000 tu, na kusema kiasi kingine
amekikata kutokana na maziwa ambayo familia yake ilikuwa ikichukua.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni