.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 18 Februari 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA NYUMBANI KWAKE UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya kumjulia hali.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni